Duration 27:33

WANAFUNZI 149 WAMETUNUKIWA SHAHADA, STASHAHADA NA ASTASHAHADA ZA CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO

224 watched
0
3
Published 28 May 2021

Jumla ya wanafunzi 149 wametunukiwa Shahada, Stashahada na Astashahada za Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA katika Mahafali ya 37 ya Katikati ya Mwaka ya Chuo hicho ambayo yamefanyika leo Mei 28. Akizungumza katika mahafali hayo yaliyofanyika katika viwanja vya Michezo vya SUA, Makamu wa Mkuu wa Chuo hicho Prof. Raphael Chibunda amesema kati ya wahitimu hao wanaume ni 92 sawa na asilimia 61.8 na wanawake ni asilimia 38.2 Wanafunzi waliotunukiwa Shahada ya uzamivu ya Udaktari wa Falsafa ni 15 kati yao wanaume wakiwa 10 na wanawake 5 huku wanafunzi waliotunukiwa Shahada ya Umahiri wakiwa 51, wanaume 23 na wanawake 28 Aidha Prof. Chibunda amewataka wahitimu kuyatumia mafanikio waliyoyapata kuwa chachu ya kuzalisha mali na kuliendeleza taifa katika sekta mbalimbali za kiuchumi Awali akizungumza katika Mahafali hayo Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Mh. Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Othman Chande amesema Baraza hilo limeisimamia ipasavyo Menejimenti ya SUA katika kutekeleza majukumu yake ya kiutafiti pamoja na kutekeleza Mpango Mkakati wa chuo hicho

Category

Show more

Comments - 0